Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye
Akiongea leo kwenye mkutano wake na waandishi wa Habari, Sumaye amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na figisu alizofanyiwa baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa.
Ameeleza kuwa alitaka kugombea nafasi ya Uenyekiti ili kuondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kua nafasi ya Mwenyekiti ndani ya CHADEMA ni ya Freeman Mbowe na haiguswi.
"Baada ya kutafakari kwa kina, ustaarabu unasema toka sasa hutakiwi, wako watakaosikitika nimelazimika kujiondoa CHADEMA kutoka leo hii, mimi sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na chama chochote, ila niko tayari kutumika na chama chochote" Sumaye - W. M Mstaafu#SumayePress pic.twitter.com/pupJhcuZjM
— East Africa TV (@eastafricatv) December 4, 2019
Pia ametaja sababu za kusitisha nia ya kugombea Uenyekiti wa Chama Taifa. 'Nasitisha rasmi safari hiyo kwa usalama wangu, usalama wa wanachama na chama chenyewe, maana Mwenyekiti Mbowe ameshasema sumu haionjwi kwa ulimi na mimi sitaki kuionja kwa sumu hiyo' - Fredrick Sumaye.
Tazama Video hapo chini akiongea.