
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Mary Masanja
Mhe.Mary amesema hayo akijibu swali la Mbunge wa Mbarali Francis Mtega aliyeuliza juu ya lini serikali italipa fidia kwa wananchi wa vijiji vitano vya Kata ya Iguva vilivyovamiwa na makundi makubwa ya tembo nakuharibu mazao yao yote hivyo kuwaweka hatarini kukumbwa na janga la njaa.
Akijibu swali Mhe.Masanja amesema, "Tumekuwa tukifanya uthamini pale ambapo kumekuwa kunatokea changamoto ya tembo kuingia kwenye maeneo ya kilimo na tunapofanya utahamini tunawalipa wa fidia kulinganana uthamini ulivyofanyika, tunalipa fidia kulingana na athari ilivyojitokeza,"
Pia Mhe.Masanja akielezea juu ya kiwango kinachotozwa cha shillingi laki moja pale ngombe moja atapoingia kwenye hifadhi amesema, "kuhusu namna ambavyo tunatoza ngome laki moja, tutambue sheria ni sisi wenyewe tumezitunga na sisi ni wataekelezaji wa sheria, Mhe.Spika na hiki kiwango kipo kwenye sheria ya wanyama sio kwamba sisi tumekiamua,"