
Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa EWURA Bw. Titus Kaguo ameiambia EATV kuwa ongezeko hilo la bei linatokana na sababu ya mabadiliko ya bei ya mafuta katika soko la dunia sambamba na kuimarika kwa thamani ya Dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania.
Aidha, Kaguo amesema bei hizo mpya haziwahusu wateja kutoka mkoa wa Tanga ambao wao wataendelea kutumia bei za mwezi uliopita kutokana na mkoa huo kuwa na bandari inayotumika kushushia na miundombinu ya kuhifadhi mafuta kiasi cha kuwa na akiba kubwa ya mafuta yaliyoingia nchini mwezi uliopita.