Tani laki 2 za miwa ya wakulima kukosa soko

Jumatatu , 25th Mei , 2020

Tani laki mbili za miwa kutoka kwa wakulima wilayani Kilombero mkoani Morogoro zinatarajiwa kubaki katika msimu wa mwaka 2020/2021 wa uzalishaji wa sukari kwenye  kiwanda cha sukari kilombero.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika

Hiyo ni kufuatia wakulima hao kuzalisha miwa tani laki nane huku uhitaji wa kiwanda hicho ukiwa ni tani laki sita pekee baada ya baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika  wilayani humo kukutana na mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania Dkt. Benson Ndiege.

Viongozi hao wamesema hali hiyo itasababisha kushindwa kurejesha mikopo yao kwenye taasisi za fedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano ya Kampuni ya Sukari Kilombero, Joseph Ngemkamu amewataka wakulima kutoongeza mashamba mingine ya miwa katika msimu huu.

Kwa upande wake mrajisi wa vyama vya Ushirika Tanzania Dkt. Benson Ndiege amesema kuwa serikali itahakikisha inawasaidia wakulima hao kadiri iwezekanavyo.