
Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo leo alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea mradi huo na kutoridhishwa nao, baada ya kukuta hauna maendeleo yoyote huku serikali ikiwa imeshalipa gharama za ujenzi.
“Ninawapa wiki moja, nataka hapa nione vifaa vyote vya ujenzi viwe vimemwagwa vywa kutosha, nataka nione mafundi wa kutosha, haiwezekani site kubwa kama hii mafundi hawafiki hata 40, kweli kazi itaenda!? Niliwaambia muongeze mafundi mwezi wa 11 lakini kwa sababu mlizozijua wenyewe hamjaongeza, sasa ndani ya wiki moja wasipoongeza mafundi, hatuwezi kuwa na mkandarasi ambaye haendani na matakwa ya mteja, nimekwisha wapatia bilioni 3 na milioni 900, nikiangalia fedha nimezitoa tangu mwezi wa 8 sioni kazi ambayo inafanana na kiwango cha fedha ambayo nimewapatia, ndani ya wiki moja wasipotimiza angalieni namna ya kuvunja huo mkataba.”, amesema Waziri Ndalichako.
Waziri Ndalichako ameendelea kwa kulalamika kuwa wakandarasi hao wamekuwa wakiaminiwa na serikali na kuwapa miradi mingi, lakini wamekuwa wakisua kukamilisha miradi kwa muda.
Ikumbukwe kwamba TBA ndio waliopewa jukumu la kusimamia ujenzi wa majengo ya hostel za Chuo Kikuu Dar es salaam, ambazo zilipata nyufa baada ya muda mfupi huku wakisema imetokana na 'expansion joint'.
