Alhamisi , 11th Jan , 2018

Baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini, Mh. Agustino Lyatonga Mrema kusema anaenda kufungua kesi ya madai ya mabilioni ya shilingi TCRA  kwa watu waliomzushia taarifa za kifo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imemuelekeza kiongozi huyo ;

kuanzia kituo cha polisi kabla ya kufika kwenye ngazi hiyo.

Akizungumza baada ya Mrema kuwasilisha malalamiko yake katika Mamlaka hiyo Naibu Mkurugenzi - Huduma za Bidhaa na Mawasiliano  Bw. Tadayo Joseph amesema kuwa Kabla ya Mrema kufika katika mamlaka hiyo alitakiwa kuanzia ndani ya jeshi la polisi kwani malalamiko hayo yanahusu kosa la jinai.

"Mzee Mrema na wananchi wengine wanaoleta taarifa za malalmiko  tunawapongeza kwa hatua hiyo. Suala ambalo alilileta ni linahusu kosa la jinai. Mamlaka hii na jeshi la polisi zinafanya kazi kwa ukaribu sana. Ameshauriwa kwanza akaripoti huko kisha atapatiwa wapelelezi kabla ya kufika kwenye mamlaka hii,".

Mrema ambaye alizushiwa kifo na watu wasofahamika siku ya Jumanne, aliahidi jana kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kwamba  angekwenda  kufungua kesi TCRA na kisha kudai Bilioni 20  kutokana na matatizo pamoja na usumbufu uliosababishwa na mzushaji wa taarifa hizo.

Mbali na hayo  Mheshimiwa Mrema jana alisema  alisema kitendo cha kuzushiwa kifo kilimsaidia kujua ni watu gani wanampenda kweli na kina nani hawampendi, kutokana na reaction zao baada ya taarifa feki za kifo chake.