Jumapili , 10th Jan , 2016

Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imeamua kuanzisha mfumo maalum wa kutathmini magonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula visivyo salama na njia za kukabiliana na magonjwa hayo .

Afisa uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Gaudensia Simwanza

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Meneja mahusiano wa TFDA Gaudensia Simwanza amesema kuwa kwa muda mrefu sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa takwimu sahihi na kwa wakati zinazohusu magonjwa yanayosababishwa na ulaji wa vyakula visivyosalama hivyo kuchelewesha kupatikana njia za kutatua matatizo hayo.

Akiyataja baadhi ya magonjwa yatokanayo na ulaji wa vyakula visivyo na ubora ni pamoja na saratani ya ini, magonjwa ya figo , magonjwa ya kuhara damu, homa ya matumbo, minyoo na amiba.

Aidha amewataka wanachi kuzingatia kanuni za afya wakati wa kuzalisha mazao ya chakula, uhifadhi wa chakula , uandaaji wa chakula na ulaji wa vyakula kwani wakati mwingine chakula kinaweza kikazalishwa kwa kufuata kanuni za afya lakini vikahifadhiwa kwa madawa ambayo yana kemikali za sumu na hatari kwa afya ya binadamu.