Jumapili , 16th Dec , 2018

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa baadhi ya mikoa nchini kutokana na vipindi vya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika siku tano zijazo.

Pichani, moja ya barabara katika jiji la Dar es salaam ikiwa imejaa maji.

Hayo yameelezwa leo Disemba 16, 2018 kati taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mamlaka hiyo, ambapo TMA imewataka wakazi wa maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kusini na karibu na Bahari ya Hindi kuchukua tahadhali hiyo.

Hii inamaanisha kuwa mafuriko yatatokea katika maeneo mengi na kuathiri jamii nzima, kuvurugika kwa usafiri na barabara kubwa kutopitika, hatari kwa maisha kutokana na maji kujaa au yanayopita kwa kasi,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kuanzia kesho Jumatatu Desemba 17, 2018 hadi Disemba 20, 2018 baadhi ya mikoa itaathiriwa na mafuriko jambo ambalo litafanya baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.