
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 2, 2021, wakati akiwasalimia wananchi wa Tegeta akiwa njiani kuelekea Bagamoyo kwa ajili ya kurekodi vipande vya filamu vitakavyotangaza utalii wa Tanzania kimataifa, filamu ambayo itazinduliwa nchini Marekani.
"Nataka niwaambie kwamba tozo zitaendelea kuwepo na sitaki kuwaficha, kwa sababu tozo zile miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya zaidi ya shilingi bilioni 60 na zimepelekwa kujenga vituo vya afya 220 hivyo tunajenga wenyewe ili wafadhili wanaokuja na masharti wasituingilie mambo yetu," amesema Rais Samia.