
Mkutano huo kwenye Ikulu ya Marekani, White House, ulifanyika kwa saa kadhaa na umetajwa na wachambuzi wa siasa kuwa moja ya juhudi kubwa kabisa za kidiplomasia kuelekea kuvimaliza vita vya Ukraine.
Rais Volodymyr Zelenskyy alikutana kwanza na Rais Donald Trump kwa mazungumzo ya wao wawili kabla ya baadaye kujiunga na viongozi wengine wa Ulaya waliosafiri kwenda Washington kumuunga mkono Zelenskyy ambaye taifa lake limo vitani.
Baada ya mazungumzo ya saa kadhaa, Zelenskyy alisema ameridhishwa na kilichoafikiwa ikiwa ni pamoja na ahadi za kuwepo hakikisho la ulinzi kwa Ukraine kutoka washirika wake wa Ulaya na Marekani pale mkataba wa amani utakapoafikiwa kati ya nchi hiyo na Urusi.
Hilo lilikuwa ndiyo suala muhimu zaidi kwa kiongozi huyo wa Ukraine ambaye nchi yake ilivamiwa kijeshi na Urusi miaka mitatu iliyopita.
Katika hatua nyingine Rais wa Marekai Donald Trump ametangaza mkutano ujao kati rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, baada ya mkutano huo wa jana Jumatatu pamoja na viongozi wa nchi za Ulaya na Umoja wa Ulaya.
Trump kupitia mtandao wake wa Truth Social amesema Baada ya mikutano hii, allimpigia simu Rais Putin na kufanya mipango ya mkutano, katika eneo litakalojulikana, kati ya Rais Putin na Rais Zelensky.
Amesema Kufuatia mkutano huu, watafanya mkutano wa pande tatu, ambao utajumuisha marais wote wawili, pamoja na yeye mwenyewe.
Hii ni hatua nyingine nzuri ya kwanza katika vita vya takriban miaka minne