Alhamisi , 29th Oct , 2020

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Dkt. Tulia Ackson, ametangazwa mshindi katika kinyang'anyiro cha Ubunge katika jimbo la Mbeya mjini, kwa kura 75,225 akiwashinda washindani wake kutoka vyama vingine vya upinzani akiwamo mshindani wake mkuu kisiasa kutoka,

Pichani ni Dkt Tulia Ackson, Mshindi mteule wa Ubunge, Jimbo la Mbeya Mjini.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Joseph Mbilinyi ''Sugu'' aliyepata kura 37,561.

Jimbo la Mbeya Mjini ni miongoni mwa majimbo ambayo yalivuta makini na hisia za wafutiliaji wengi wa siasa nchini Tanzania, kutokana na washindani hao kuonekana kuwa na mvuto, ushawishi na nguvu za kisiasa zinazoelekeana.
Joseph Mbilinyi “Sugu” amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa misimu miwili 2010 hadi 2020, huku Dkt. Tulia akiingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli na baadaye kuwa Naibu Spika.

Ikumbukwe kuwa Joseph Mbilinyi, ndiye aliyekuwa mbunge pekee kwa uchaguzi wa mwaka 2015, kupata kura nyingi zaidi kulikoni wagombea wengine wa ubunge, ambapo Sugu alipata kura 97,675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyego Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46,894.