Jumanne , 11th Nov , 2025

Mnamo Novemba 7, 2025 Niffer na wenzake walifikishwa mahamani hapo na kufunguliwa mashtaka ya uhaini. 

Wakati leo kesi ya uhaini inayowakabili mfanyabiashara Jeniffer Jovin ikiunguruma katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wakili Peter Kibatala amesema kwa kushirikiana na mawakili wengine watatoa huduma ya kisheria kwa Mfanyabiashara huyo, Jenifer Jovin pamoja na Ruthimelda Born Gregory  na wenzao wengine 20 wanaokabiliwa na kesi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Wakili Peter Kibatala amesema washtakiwa hao mahakamani na badala yake wameshiriki kwa njia ya mtandao.

Mawakili wa utetezi(upande wa Niffer na wenzake) uliwasilisha hoja kuu mbili mahakamani hapo ya kwanza ni kuwa wateja wao waliteswa na kupigwa hivyo wapatiwe matibabu hoja ambayo ilikubaliwa na hoja ya pili ni kuwa hati ya mashtaka si halali ambayo upande wa jamhuri uliomba kuijibia leo Novemba 11,2025.

Mnamo Novemba 7, 2025 Niffer na wenzake walifikishwa mahamani hapo na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.