"Tulijua tutashinda" – Pole Pole

Jumapili , 18th Feb , 2018

katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole, amesema chama cha Mapinduzi (CCM) kilijua kuwa kitashinda kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Polepole amesema watu wameiamini CCM kwa sababu inawajibika kwao, hivyo ahlikuwa suala humu wao kupatra ushindi.

“Niwashukuru kwa kujitokeza, niwashukuru kwa kuwa watulivu, wananchi wengi walionyesha kiu yao ya kupata wawakilishi ambao watwachagua wenyewe, wengi wao walieleza wanapenda kuona kazi nzuri ambayo Rais anaifanya inafanyika katika majimbo hayo, matokeo yameeleza sauti ya watanzania katika maeneo haya, CCM kwa mara nyingine tumeshinda kwa kishindo, sisi tulijua kuwa tutashinda, kwa sababu ya kazi nzuri ambayo serikali ya CCM ilikuwa ikiifanya”, amesema Humprey PolePole.

Licha ya hayo Pole pole amesema kuwa kitendo cha vurugu kilichotokea pia walijua kuwa wapinzani wataleta vurugu, kwani kufanya vurugu ndio kawaida yao.