
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana Dkt John Pombe Magufuli.
Katika makubaliano hayo serikali ya Tanzania imefanikiwa kumiliki asilimia 49 ya hisa za kampuni hiyo, zikipanda kutoka asilimia 40 walizokuwa wakimiliki awali huku wamiliki wenza wakimiliki asilimia 51 tu ya hisa zote.
Akizungumza mara baada kushuhudia hafla hiyo ya utiaji saini, Rais John Magufuli amesema, "serikali inapolalamika kitu hailalamiki kutoka hewani na bahati nzuri tunawasomi wazuri mno ila tulikuwa hatuwatumii, tunawapuuza ila huu ndiyo uwe mwanzo wa kuwaheshimu watu wetu tusipowaheshimu tutanedelea kulaliwa".
"Hili ni ushindi kwa Taifa letu ni ushindi mkubwa kwa Watanzania na ushindi mkubwa kwa Airtel, kwa mtu mwingine angesimama angesema hatutaki wawekezaji ila tunataka ndiyo maana tuna Center kabisa ya uwekezaji," ameongeza Rais Magufuli.