Ijumaa , 10th Oct , 2025

Maria Corina Machado kutoka Venezuela ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel 2025 Kutokana na  kazi ya kukuza haki za kidemokrasia nchini Venezuela.

Machado ameshinda kwa kuendeleza haki za kidemokrasia bila kukoma

Katika chapisho kwenye mtandao wa X, kamati hiyo inasema imemtunuku Maria Corina Machado Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kazi yake bila kukoma ya kuendeleza haki za kidemokrasia kwa watu wa Venezuela na kwa mapambano yake ya kufikia mabadiliko ya haki na amani kutoka kwa udikteta hadi demokrasia

Machado 'amekuwa mtu muhimu wa kuunganisha'

Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2025 inaenda kwa "mwanamke ambaye anaendeleza harakati za kupatikana kwa demokrasia, katikati ya giza linaloongezeka".

Maria Corina Machado anapokea tuzo ya Amani ya Nobel kwa kuwa mmoja wa "kupigiwa mfano" kwa ujasiri katika Amerika ya Kusini siku za hivi karibuni.

Machado amekuwa mtu muhimu wa kuunganisha watu, mwenyekiti wa kamati anaongeza.