Jumatano , 17th Dec , 2025

Uamuzi huo utatolewa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Dk. Juliana Massabo katika kesi ambayo Madeleka alihoji uhalali wa tangazo la serikali la kufutwa kwa sherehe za uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika (Tanzania Bara) za mwaka huu (2025).

Uamuzi katika kesi iliyofunguliwa na Wakili Peter Madeleka dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kufutwa kwa Sherehe za Uhuru 2025, unatarajiwa kutolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma, leo Desemba 17, 2025.

Uamuzi huo utatolewa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Dk. Juliana Massabo katika kesi ambayo Madeleka alihoji uhalali wa tangazo la serikali la kufutwa kwa sherehe za uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika (Tanzania Bara) za mwaka huu (2025).

Mbali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) anashtakiwa pia katika kesi hiyo.

Awali, kesi hiyo ilitajwa Ijumaa Novemba 28, 2025 Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa chini ya Jaji Mfawidhi a Mahakama Kuu Dodoma Dkt. Juliana Masabo, kabla ya kuahirishwa tena hadi Disemba 2, 2025, kabla ya serikali kuwasilisha pingamizi la kesi hiyo kufutwa bila kusikilizwa.

Shauri hilo linafuatia tamko la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa kwenye ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam aliloutangazia umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza fedha zilizokuwa zimeandaliwa kwaajili ya sherehe za uhuru (09 December) mwaka huu (2025), kuelekezwa kwenye kushughulikia ukarabati/ ujenzi wa miundombinu ya umma iliyoharibiwa kufuatia vurugu zilizotokea Oktoba 29 mwaka huu, vurugu zilizopelekea uharibifu wa mali za umma na binafsi, majeruhi na vifo.