
Gaudencia Kabaka waziri wa kazi na ajira ambae pia anawania kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge jimbo la Musoma Mjini
Wagombea wawili walitumiwa kuhusika kuingiza kataratasi za kupiga ambazo tayari zimewapa ushindi na kusababisha uchaguzi huo kuhairishwa wameibuka na kudai hujuma hiyo imefanywa na wapinzani wao.
wagombea hao Mh Nyambari Nyangwine wa jimbo la Tarime Vijijini na Mh Gaudencia kabaka wa jimbo la Tarime Mjini wamedai kuwa hawahusiki na kuingiza karatasi hizo ambazo zimekamatwa zikiwa zimepigiwa kura katika majina yao ali kitendo hicho kimefaganywa na wapinzani wao kwa lengo la kuwachafua.
Katika matokeo ambayo yametangazwa katika majimbo ya Musoma mjini Vedastus Mathayo ,jimbo la Butiama Mh Nimrod Mkono jimbo la Mwibara Mh Kangi Lugola akitangazwa kuwa mshindi pamoja na jimbo la Serengeti Dk Steven Kebwe, Mh Lameck Airo wa jimbo la Rorya akitangazwa kupata ushinda mkubwa kwa kuwashinda wagombea wengine kumi na tatu.