
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Kulia ni Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli
Rais Museveni ameandika hayo katika ukurusa wake wa Twitter na kutoa pole kwa Watanzania kufuatia msiba huo mzito huku akimpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akimuelezea Hayati Dkt. Magufuli amesema alikuwa ni rafiki wa ukweli kwa Uganda, bingwa wa kujitoa katika upatanishi wa uchumi wa Afrika Mashariki na maendeleo, mwenye msimamo wa wazi wenye kutia nguvu katika masuala ya Tanzania na Afrika.
Sambamba na hayo Rais Museveni amesema nchi ya Tanzania itaukumbuka uongozi wake uliotukuka na mchango wake ambao walikuwa wanautengea kwa muhula wake wa mwisho katika nafasi yake ya uongozi.