
Akizungumzia hilo, Kamishina wa Uraia na Pasipoti, Gerald Kihinga amesema idara hiyo ina dhamana ya kuchunguza na kuthibitisha uraia wa mtu yoyote anayetiliwa mashaka na kwamba walishawahi kumtumia wito wa kumuita mara nyingi lakini hakuwahi kufika na ndipo waliposhirikiana na polisi na kumkamata.
"Suala hili limekuwa ni kubwa sana kwa sababu ni mwandishi wa habari lakini tunao watu wengi sana tunawahoji, maadili yangekuwa yanaruhusu kusema ningewatajia watu wote tunaowahoji, wapo wengi sana nikianza kuwatajia hapa mtashangaa. Vitu hivi haviko wazi kwasababu watu hawa hawajitangazi wala kukimbia, wamekuwa wakitupa ushirikiano tofauti na bwana Kabendera", amesema Kamishna Kihinga.
Mwandishi wa habari Erick Kabendera alikamatwa kwa nguvu na watu waliojitambulisha kama polisi siku ya Julai 29 nyumbani kwake Mbweni Jijini Dar es Slaam, Julai 30 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya DSM, SACP Mambosasa alikiri Jeshi la Polisi kumkamata mwandishi huyo.