Jumatatu , 9th Jan , 2023

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amekanusha taarifa zilizoenea kuwa aliyekuwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ana mpango wa kujiuzulu wadhifa wake kama mwenyekiti wa baraza la uongozi la Azimio la Umoja One Kenya

Odinga amesema madai hayo ni propaganda zinazoundwa na vyombo vya habari nchini humo zenye lengo la kufifisha nguvu ya Azimio katika kuwatetea wakenya

"Yeye (Uhuru) yuko Azimio bado, nilikuwa na Uhuru nilikuwa naye na tumezungumza, bado ni Mwanachama na ni sehemu ya uongozi wa Azimio" amesema Odinga

Wiki iliyopita nchini Kenya zilisambaa taarifa kwenye vyombo vya habari zikieleza kuwa Rais huyo mstaafu wa Kenya anajiandaa kutangaza kujitoa kwenye umoja huo wa Azimio