Zinedine Zidane
Kipaombele cha rais Florentino Perez ni kurejesha Madrid katika hali nzuri iliyokuwa ndani ya kikosi hicho chini ya uongozi wa Carlo Ancelotti. Ili kufikia hili, chaguo lake analopendelea ni mtu ambaye ametoa matokeo bora kwake katika vipindi mbalimbali, Zinedine Zidane .
Suala la Mfaransa huyo ni kwamba tayari amekubali kuinoa Ufaransa baada ya Kombe la Dunia la 2026, lakini nia ya rais huyo kwa takriban mwezi mzima sasa imekuwa ni kumweka kuinoa timu katika kipindi hiki kigumu.
Ikiwa chaguo la Zizou litashindikana, wa pili katika mstari wa kurithi nafasi ya Alonso atakuwa mchezaji mwingine wa zamani, Alvaro Arbeloa , ambaye anafanya kazi nzuri katika msimu wake wa kwanza wa kuinoa Castilla
Bado haijafahamika ni nani atakuwa kocha ajaye wa Real Madrid, lakini dalili zote zinaonyesha Alonso kuhesabu siku za kuaga sura ambayo haijapita kama alivyotarajia.



