Rekodi 10 za soka
Hizi hapa rekodi 10 za soka ambazo wengi hawazifahamu;
- Neymar Alifika Top 10 kwenye tuzo za Ballon d’Or akiwa anacheza nje ya Ulaya (Santos FC)
- Cristiano Ronaldo mwaka 2016 alishinda mataji mingi kuliko idadi ya mechi alizopoteza (Mataji 4, kupoteza mechi 3)
- Lionel Messi ndiye mchezaji pekee aliyeshinda tuzo ya Ballon d’Or katika Miongo mitatu Tofauti.
- Antonie Griezmann hajawahi kushinda kombe la ligi kuu ya Nchini Uhispania (La Liga) akiwa katika Klabu ya Atletico Madrid
- Mwaka 2005 Kocha Jose Mourinho akiwa katika Klabu ya Chelsea aliweka rekodi ya kuruhusu magoli 15 pekee EPL.
- Aberdeen FC ndiyo Klabu ya mwisho kuifunga Real Madrid kwe fainali ya UEFA CL 1983
- Hakuna Kocha yeyote Muingereza aliyefanikiwa kushinda Kombe la Ligi kuu ya nchini Uingereza EPL
- Mohamed Salah alishinda tuzo ya goli bora la mwaka 2018 lakini goli hilo halikushinda tuzo ya goli bora la mwezi EPL.
- Cristiano Ronaldo hajacheza katika Ligi kuu ya Nchini Ujerumani lakini amefunga magoli mengi dhidi ya golikipa Manuel Nuer
- Diego Maradona amewahi kucheza katika Klabu ya Tottenham Hotspur




