Barabara hiyo ilitengewa kiasi cha shilingi bilioni 4 zilizokuwa zitumike katika sikukuu ya Uhuru Disemba 09.12.2015 na kuamriwa na Rais Dkt. John Magufuli kutumika kutengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kusaidia kupunguza msongamano wa magari na hasa kupoteza muda wa kufanya kazi katika barabara hiyo.
Kwa sasa barabara hiyo imekwisha kamilika katika hatua ya lami kwa kipande cha barabara kutoka mwenge hadi sayansi na mafundi wa TANROADS wanaendelea na ujenzi kukamilisha eneo lilobakia .
Aidha kasi ya ujenzi wa barabara hiyo umeonekana kuwa na kasi kutokana na mafundi kugawiana vipande vipande na vifaa ili kufanya kazi hiyo kukamilika kwa wakati kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.