Jumanne , 1st Sep , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanajaro Anna Mghwira, amewataka wanasiasa kujifunza kujenga hoja na si kuigeuza mijadala ya kisiasa kuwa ugomvi.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.

Amesema hayo leo Septemba 1, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo amesema kampeni zinaendelea hivyo watu wanaopenda siasa kujifunza kubishana kwa hoja kama hawawezi waachane na siasa.

“Kampeni zimeanza na zinaendela,watu wanapenda siasa lakini mijadala ya kisiasa wanaifanya ugomvi, ukipenda siasa jifunze kujenga hoja, bishana kwa hoja usigombane, shiriki, usikabili, kuwa na umakini na usikurupuke, ukishindwa haya acha siasa", amesema Anna Mghwira.