Jumanne , 4th Aug , 2015

Ukosefu wa mawasiliano katika baadhi ya maeneo mkoani Mtwara imetajwa kuwa ndio sababu iliyochang

Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Bw. Shaibu Akwilombe akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika uwanja wa Fisi.

Ukosefu wa mawasiliano katika baadhi ya maeneo mkoani Mtwara imetajwa kuwa ndio sababu iliyochangia ucheleweshaji wa kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni za uchaguzi kwa wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani.

Hayo yamezungumzwa jana na katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo, Shaibu Akwilombe, alipokuwa akitangaza matokeo ya awali ya majimbo sita kati ya tisa yaliyofanya uchaguzi.

Uchaguzi pia uligubikwa na udanganyifu wa hapa na pale ambapo mgombea mmoja alikutwa na karatasi ambazo zimeshtiwa tiki ofisini kwake ambapo hata lipoulizwa alikana kuzijua karatasi hizo.

Aidha, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, George Mkuchika amefanikiwa kushinda katika jimbo la Newala mjini ambalo lilikuwa likiwaniwa na makada watatu huku Asnain Murji akishinda katika jimbo la Mtwara mjini kwa kura 10,055.