
Waziri wa katiba na sheria nchini Tanzania, Dkt Asha-Rose Migiro. Wizara yake ina jukumu la kuhakikisha haki inapatikana kwa makundi yote katika jamii.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar-es-Salaam na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu nchini Tanzania Jaji Euserbia Munuo wakati akizindua namba maalum ya simu itakayopigwa bure kwa lengo la kupata msaada wa kisheria bure, iliozinduliwa na kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC).
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa WLAC, Theodesia Muhulo amesema kumekuwa na mwamko mkubwa kwa sasa wa wananchi kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na hivyo kupitia WLAC wanawake wataweza kupata msaada wa kisheria bure pale wanapokumbana na vitendo vya ukatili.