Jumatatu , 12th Sep , 2022

Muungano wa chama cha upinzani cha  CCC nchini Zimbabwe umesema kwamba kiongozi wake Nelson Chamisa amenusurika jaribio la mauaji baada ya msafara wake kushambuliwa na bomu katika mji wa  Chinhoyi.

 Mji wa Chinhoyi  upo umbali wakilomita 115 kufikia mji mkuu wa  nchi hiyo Harare.

Katika tamko lao walilolitoa kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Muungano huo umesema kwamba Kiongozi wao Nelson Chamisa  alilengwa kushambuliwa na msafara wake kwa kutumia milipuko wakati akikaribia ukumbi mmoja wa mkutano mjini humo.

Taarifa ya CCC imeongeza kuwa Ukumbi huo pia ulilipuliwa na bomu la petrol jumamosi ya juzi yna watu wasiojulikana. Chama hicho kimepeleka lawama zake kwa wale iliyowaita vijana wa  chama tawala nchini humo  Zanu-PF  kwa mashambulizi hayo. Serikali haijajibu lolote kuhusiana na madai hayo. 

Shambulizi hilo limetokea ikiwa ni wiki kadhaa zimepita toka Bwana  Chamisa ashambuliwe yeye na msafara wake na vijana wanaosaidikwa kuwa anatokea chama tawala. Joto la kisiasa lipandana nchini Zimbabwe  kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.