Jumamosi , 29th Jan , 2022

Askofu Mkuu wa WAPO Mission International, Sylvester Gamanywa, amesema kuwa Samia Suluhu Hassan ni Rais wa kwanza ambaye ameshika madaraka hayo bila kupitia mifumo ya Marais wengine wote waliomtangulia na hakuna malalamiko yoyote kwamba yupo hapo kwa njia ya mashaka.

Askofu Mkuu wa WAPO Mission International, Sylvester Gamanywa,

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 29, 2022, wakati wa  kongamano la kumtakia heri ya kuzaliwa na Baraka za mwaka mpya Rais Samia, lililoandaliwa na viongozi mbalimbali wa dini na kusema kwamba Rais Samia yupo madarakani kwa sababu amesukwa hivyo na Mungu tangu akiwa tumboni mwa Mama yake.

"Urais wa Samia hauna mgogoro na hakuna malalamiko yoyote kwamba amekuwepo pale kwa nia ambayo ina mashaka mashaka, na toka amekuwa Rais nchi imetulia kana kwamba hakuna kilichotokea," amesema Askofu Gamanywa