Jumatano , 8th Jun , 2022

Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mtwara, umetoa wiki moja kwa mamlaka husika kuhakikisha wanawachukulia hatua watuhumia wote wanaohusika kwenye myonyoro wa uuzaji wa pembejo feki, na kwamba endapo mamlaka zitashindwa kuwachulia hatua, wapo tayari kuwataja kwa majina wale wote wanaohusika.

Korosho

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti, ametoa saa 48 kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Makonde Sulfa inayodaiwa kusambaza pembejeo feki za zao la korosho kujisalimisha kwa jeshi la polisi mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa huo amesema mbali na kujisalimisha kwa mfanyabiashara huyo, ambae anadaiwa kuuza pembejeo zisizofa kwa wakulima, tayari mamlaka zinawashikilia watu saba wanaodaiwa kuhusika na sakata hilo.