
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohammed Kawaida
Kauli yake hiyo inatokana na kile alichokieleza kuwa, taarifa waliyonayo vijana wengi ni kwamba lazima uwe na elimu ya kidato cha nne ndipo upate nafasi katika mradi huo.
Kawaida ametoa kauli hiyo jijini Dodoma alipotembelea mradi wa BBT kituo cha Bihawana ikiwa ni ziara yake ya kikazi.
"Ukweli ukienda shambani utakuta wanaolima ni wale wenzangu na mimi wa darasa la saba, kidato cha pili na wengine, tukitangaza wanaohitajika ni kidato cha nne tutawanyima fursa hawa wengine, jeshini wanataka kidato cha nne, kila eneo kidato cha nne hili kundi lingine tunalipeleka wapi," amesema Mwenyekiti huyo.
Akizungumza kuhusu kigezo cha kidato cha nne, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli, amesema makundi yote ya vijana yana nafasi ya kuomba fursa hiyo.
"Tumezingatia na tutazingatia makundi yote ya vijana kupata nafasi katika mradi huu kwa hiyo kila kijana anayo fursa," amesema.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Kituo hicho cha mafunzo, Asia Msuya amesema kinachofanyika katika mafunzo hayo ni kinyume na inavyoaminiwa na baadhi kwa kusema wapo wanaoamini kuwa mradi huo unafanyika kisiasa, lakini uhalisia ni kinyume chake, kwani wanajifunza kwa kina kuhusu kilimo.