Jumatano , 30th Jul , 2025

Mradi wa GAIN unalenga kuwawezesha vijana kushiriki kwa dhati katika sera, mikakati na utekelezaji wa mabadiliko ya mifumo ya chakula kwa mustakabali bora wa kizazi cha sasa na kijacho.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amewataka vijana kutumia fursa ya Mkutano wa Pili wa Mfumo wa Chakula wa Umoja wa Mataifa kwa kuleta mawazo bunifu na kuongoza kwa vitendo mageuzi ya mifumo ya chakula yenye lishe bora, salama na endelevu nchini Tanzania.

Waziri Kombo amezungumza hayo katika Mkutano wa Pili wa Mfumo wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (UNFSS+4) uliofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 27 hadi 29 Julai 2025 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Pia, amekutana na vijana viongozi kutoka Tanzania wanaoshiriki katika mageuzi ya mifumo ya chakula kupitia mradi wa Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN) chini ya kampeni ya Vijana4Food na kuwaambia kuwa vijana hao ni sauti muhimu ya vijana wa Tanzania kwenye majukwaa ya kimataifa.

Mradi wa GAIN unalenga kuwawezesha vijana kushiriki kwa dhati katika sera, mikakati na utekelezaji wa mabadiliko ya mifumo ya chakula kwa mustakabali bora wa kizazi cha sasa na kijacho.