Ametoa kauli hiyo mjini Sumbawanga wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki Kumi na Mbili (12) kwa maafisa lishe wa halmashauri zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la udumavu ambao kwa Rukwa upo asilimia 47.9 kwa takwimu za mwaka 2018.
Sendiga amebainisha kuwa maadhimisho hayo yakifanyika itakuwa jukwaa zuri la wataalam wa lishe kutoa elimu ya uandaaji vyakula bora na ulaji sahihi kwa kutumia vyakula vinavyopatikana kwenye mazingira ya Rukwa kwa kuwa mkoa huo ni mzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula.