
Kuna taarifa pia kuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa nao wamezuiwa kufika katika nyumba ya mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini humo Bw. Etienne Shishekedi.
Hatua ya kuongezwa ulinzi kwenye nyumba ya Bw. Shishekedi inatokana na madai ya mara kwa mara ya kiongozi huyo wa upinzani kutaka Rais Joseph Kabila aondoke madarakani pindi muhula wake utakapokamilika mwezi ujao.
Hata hivyo Rais Kabila amesisitiza kuwa uchuguzi huo wa mwezi Disemba lazima uahirishwe huku akimteua mwanasiasa wa upinzani Bw Samy Badibanga kuwa waziri mkuu mpya.
