Jumatatu , 29th Jun , 2015

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa chama hicho kushughulikia matatizo ya Wananchi badala ya kufanya vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kugombe madaraka.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdrulrahman Kinana akizungumza wakati wa mapokezi yake kuingia mkoa wa Mwanza.

Akiwa katika Ziara yake jijini Mwanza jana kinana amewaambia wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya hiyo kuwa ni vyema wakashiriki kikamilifu kwenye masuala yanayowagusa wananchi ili kuendelea kuitekeleza ilani ya CCM,

Kinana amewataka wajumbe hao watumie muda mwingi kushughulikia kero za wananchi pamoja na kutafuta ufumbuzi kwa mambo yanayoshindikana kuliko kukaa kusuluhisha migogoro ya ndani inayotokana na kugombea madaraka.

Aidha katibu huyo aliongeza kuwa wale wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali waachwe wawanie nafasi hizo ili kukipatia chama ushindi na wale ambao hawana sifa wawaachie wanaokubalika zaidi.