Jumamosi , 10th Jan , 2015

Rais Jakaya Kikwete amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kuliombea taifa na watanzania kwa ujumla ili waweze kukabiliana na majukumu yao kwa amani

Sehemu ya viongozi wa dini na waumini waliohudhuria hafla hiyo

Rais Jakaya Kikwete amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kuliombea taifa na watanzania kwa ujumla ili waweze kukabiliana na majukumu mengi na makubwa yaliyoko mbele yao kwa amani na utulivu likiwemo la kupata katiba mpya.

Katika salam zake kwenye hafla ya kumsimika Askofu Solomon Masangwa wa Dayosisi ya Kaskazin Kati zilizowasilishwa na waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt Marry Nagu Rais Kikwete amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa kuwawezesha viongozi wa dini kutimiza wajibu wao .

Akizungumza baada ya kusimikwa Askofu Solomon Masangwa amesema kazi kubwa aliyonayo ni kudumisha umoja na mshikamano na kuendeleza yote yaliyoachwa na aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo marehemu Thomas Laizer.

Katika salam zao mkuu wa kanisa hilo nchini Askofu Dkt Alexs Malasusa aliyewawakilisha viongozi mbalimbali wa dini na waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa aliyewawakilisha viongozi wa kisiasa wamewaomba waumini wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla kudumisha ushirikiano na upendo miongoni mwao na kwa viongozi wao.

Katika hafla hiyo pia imehudhuriwa waziri mkuu mstaafu Fredrik Sumaye, Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Lazaro Nyalandu , wabunge, mabalozi na maaskofu kutoka makanisa mbalimbali.