Jumamosi , 16th Jan , 2016

Viongozi wa umma 3,709 hawajarejesha fomu za tamko la rasilimali na madeni kama ambavyo sheria ya maadili ya viongozi wa umma, inavyotaka kufanya hivyo.

Hayo yameelezwa na kamishna wa maadili wa sekretariati hiyo, Jaji Mstaafu Salome Kaganda, katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

“Hadi kufikia Desemba 31, 2015 jumla ya viongozi 11,428 ndio waliorejesha matamko yao kwa kamishna wa maadili huku viongozi 3,709 hawajatimiza wajibu huo wa kisheria na hatua zitachukuliwa dhidi yao,” amesema Jaji Kaganda.

Vivyo hivyo serikali imeanzisha utaratibu wa viongozi na watumishi wote wa umma ambao wako katika mihimili mitatu inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani Serikali, Bunge na Mahakama kutia saini fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wote na watumishi wote wa umma.