Jumamosi , 14th Sep , 2019

Viongozi wanne wa Chama cha ACT Wazalendo akiwemo Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma Taifa Ado Shaibu, wamekamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Temeke kwa kile kilichoelezwa walikuwa wanafungua matawi bila kuwa na kibali.

Bendera ya ACT Wazalendo

Tamko la chama hicho limetolewa leo Septemba 14  na M/kiti Kamati ya Itikadi, uenezi na mawasiliano Salim Bimani, ambapo ameeleza kutofurahishwa na kitendo hicho kwani ni kuingiliwa kwa masuala ya vyama vya siasa na kuvizuia kutekeleza majukumu na wajibu wao kisheria.

Bimani ameliomba  jeshi la Polisi liwaachie viongozi hao na lisimamie wajibu wake wa kulinda usalama na Mali za Raia, badala ya kuwa sehemu ya Chama.

Waliokamatwa ni pamoja na Katibu wa Itikadi, uenezi na Mawasiliano Kwa Umma Taifa  Ado Shaibu, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam Soud Salum, Katibu wa Uchaguzi Mkoa Risasi Semasaba na Katibu wa Ngome ya Vijana wa Kata ya Azimio anayejulikana kwa jina la Said.