Jumapili , 11th Dec , 2022

Maafisa wa Chile wametoa tahadhari  ya usalama baada ya volkano kulipuka umbali wa mita 6,000 (karibu futi 20,000) angani.

Volkano ya Lascar, ambayo iko katika Andes, iligonga mwamba siku ya Jumamosi, na kusababisha mitetemeko midogo ya ardhi.

Hakuna uharibifu katika eneo linalozunguka hadi sasa umeripotiwa, lakini onyo la awali  limetolewa.

Huduma ya Kitaifa ya Jiolojia na Madini ya Chile imesema kwamba mlipuko huo unaweza kutokea muda wowote. Wwataalamu nchini humo wanafuatilia eneo la milipuko midogo na muonekano wa moshi,  

Wakazi wa  Talabre, katika mji mdogo wa  Antofagasta,ambao upo umbali wa  kilomita 12 (maili 7) kutoka volkano, walikua wa kwanza kugundua viashiria vya mlipuko huo.