Jumatatu , 30th Aug , 2021

Zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa vyenye usajili kamili limeanza leo Agosti 30, 2021.

Nembo za vyama vya CCM na CHADEMA

Kwa mujibu wa barua na ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kusainiwa na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, zoezi hilo litaanza kwa
kuhakiki vyama vyenye ofisi zake Jijini Dar-es-salaam. 

Vyama vitakavyofungua zoezi hilo ni AAFP kuanzia saa 2:00 asubuhi na NRA 6:30 mchana. Siku ya Jumanne zoezi hilo litaendelea kwa kuhakiki vyama vya UDP na NLD, vikifuatiwa na vyama vya UMD na ADC siku ya Jumatano ya tarehe 1 Septemba, 2021.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 2 Septemba, 2021 vyama vya CCK na Demokrasia Makini vitafanyiwa uhakiki. Siku ya Ijumaa itakuwa zamu ya chama cha CHADEMA na
UPDP.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo zoezi la uhakiki litaendelea wiki inayoanza tarehe sita kwa kuhakiki vyama vya NCCR na CHAUMA kuanzia saa mbili na nusu asubuhi.

Vyama vingine vitakavyohakikiwa wiki hiyo ni pamoja na vyama vya ACT- Wazalendo, CUF, TLP, SAU, ADA TADEA na DP. Uhakiki wa Chama cha Mapinduzi (CCM) utafanyika Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dodoma siku ya Ijumaa ya tarehe 10 Septemba, 2021.