
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ni mmoja wa walioikosoa bajeti hiyo kwa madai ya kuwa ya upendeleo.
Wakichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maji katika kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma wabunge hao wamesema wananchi wamekuwa wakitafuta maji kwa kwenda umbali mrefu huku wakina mama na wanawake wakiwa ndio wahanga wakubwa wa tatizo hilo.
Wamesema ni wakati muafaka sasa kwa serikali kuona umuhimu wa tatizo hilo kwa lengo la kuongeza bajeti katika Wizara ya Maji ili kupunguza kero ya maji kwa wananchi hasa wale wa maeneo ya vijijini.