Jumatatu , 14th Dec , 2015

Uchaguzi mkuu wa ubunge katika jimbo la Arusha mjini umefanyika kwa amani, huku idadi ya wapiga kura waliojitekeza ikiwa ndogo kulinganishwa na chaguzi zilizopita.

Msimamizi wa Uchaguzi kata ya Themi, Esther Kashangaki

Uchaguzi huo unafanyika ikiwa ni zoezi la kukamilisha uchaguzi mkuu octoba 25 mwaka huu, kufuatia kifo cha mgombea wa ubunge wa chama cha ACT wazalendo Estomih Mallah, aliyefariki siku chache kabla ya uchaguzi.

Wapigakura waliondikishwa kwenye daftari katika jimbo la Arusha Mjini ni laki tatu kumi na saba elfu mia nane na kumi na nne huku taswira ya awali inaonesha idadi ndogo ya wapiga kura tokea kufunguliwa kwa vitua saa moja asubuhi hadi kufungwa kwake majira ya saa kumi jioni

Wagombea wanaoshiriki katika uchaguzi huo ni pamoja na Godbless Lema wa cha cha demokrasia na maendeleo Chadema anayejaribu kutetea kiti hicho baada ya kuongoza kwa miaka mitano.

Mgombea mwingine ni Philemon Mollel kupitia CCM aliyepiga kura katika kituo cha shule ya sekondari kimandolu kata ya kimandolu.

Zuberi Mwinyi mgombea kupitia chama cha wananchi Cuf aliyepiga kura katika kituo cha YMCA daraja mbili.

Mwingine ni mgombea pekee mwanamke Navoi Mollel kupitia chama cha ACT Wazalendo aliyepiga kura katika kituo cha Burka shuleni katika kata ya Olasiti.

Katika uchaguzi huo unaofanyika katika vituo 721 kwenye kata 25 za jimbo la Arusha mjini, baadhi ya wapiga kura wamesema mazingira ya zoezi hilo ni tulivu.

Hadi tunakwenda mitamboni matokeo rasmi ya uchaguzi huo yalikuwa bado hayajatangangazwa ambapo tofauti na ilivyozoeleka matokeo kujumuishwa na kutangazwa katika ofisi za halmashauri ya jiji safari hii zoezi hilo linafanyikia katika eneo la Chuo cha VETA Kata ya Engutoto Nje kidogo ya Jiji la Arusha.