Jumatatu , 26th Jul , 2021

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wafanyabiashara waliokimbilia Nakonde nchini Zambia, kwa maelezo ya kuwa huko kuna unafuu wa kodi kuliko Tunduma nchini Tanzania warejee na malalamiko yao yatafanyiwa kazi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba

Dkt. Nchemba ameitoa kauli hiyo Mjini Tunduma wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji huo wakiwemo wafanyabiashara katika mpaka huo wa Tanzania na Zambia walioeleza kero zao mbalimbali.

"Wewe Mtanzania wala usiikimbie nchi yako tutarekebisha yale yaliyomatatizo lakini kama umepata fursa ya kuwekeza wekeza inaruhusiwa, lakini usiikimbie nchi yako sababu ya matatizo hayo tutayarekebisha," amesema Waziri Dkt. Nchemba.