Alhamisi , 18th Feb , 2016

Wananchi wa Uganda leo wanatimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua Rais na wabunge katika uchaguzi ambao wapiga kura milioni 15 wanatarajiwa kupiga kura katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa moja na vitafungwa saa kumin alasiri ili kupisha zoezi la kuhesabu kura hizo ili kuweza kumpata mshindi wa uchaguzi huo.

Wagombea urais wapo 8 viti vya ubunge ni 290 vituo vya kupigia kura ni 28,010 na wapiga kura waliosajiliwa 15,277,196 ambapo Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni ambaye ametawala taifa hilo kwa miaka 30 naye ni mmoja wa wagombea Urais.

Aidha Mwangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo yupo katika taifa hilo akizunguka katika vituo mbalimbali kujionea hali halisi ya namna zoezi la upigaji kura na upatikanaji wa matokeo litakavyokwenda.

Chanzo BBC