Jumatano , 2nd Jan , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Januari 02 Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim anayepatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam baada ya kufanyiwa upasuaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimjulia hali hali Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.

Aidha Rais Magufuli pamoja na kutoa pole kwa Dkt. Salim, akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wameongoza sala ya kumuombea kiongozi huyo mstaafu.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha siku 4 ambapo Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kuwatembelea wagonjwa ambapo Decemba 30, 2018 kiongozi huyo wasaidizi walifika hospitali kwa kumjulia hali Mama yake Mzazi.

Suzana Magufuli anapatiwa Matibabu Jijini DSM anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ambapo amekuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu sasa.