Jumapili , 2nd Apr , 2023

Wanaume watatu wa Uingereza, akiwemo mfanyakazi wa hisani, wanashikiliwa katika mahabusu ya Taliban nchini Afghanistan, shirika lisilo la kiserikali la Uingereza linasema, na wizara ya mambo ya nje ya Uingereza inasema inafanya kazi ili kupata mawasiliano nao.

 

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, wizara ya mambo ya nje ilisema inatoa msaada kwa familia zao.

Mtandao wa Presidium umesema unawasaidia wafungwa wawili, daktari wa hisani Kevin Cornwell, 53, na mtu ambaye hakutajwa jina.

 Taarifa zinasema kuwa Wanaume hao walikamatwa na polisi wa siri wa Taliban Januari 11.   

Mwaka jana, Taliban ilimwachilia huru mpiga picha mkongwe wa televisheni na raia wengine wanne wa Uingereza ambao ilikuwa imewashikilia kwa miezi sita.