Alhamisi , 22nd Oct , 2015

Kufuatia kutoelewana kuhusu suala la kusimama umbali wa mita 200 kutoka eneo la kupigia kura, baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mtwara Mikindani wameanza kushikwa na hofu juu ya usalama wao kiasi cha kulazimika kukimbia mji.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo

Kwa mujibu wa mashuhuda waliopo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani humo, wamesema kuanzia jana asubuhi kumekuwa na idadi kubwa ya wasafiri wanaotoka mjini Mtwara kuelekea sehemu mbalimbali hasa wilayani, kuliko wanaoingia mjini.

Awali akizungumza katika kikao na waandishi wa habari juu ya kuwahamasisha wananchi kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, aliwataka wananchi kuondoa hofu juu ya kutokea kwa vurugu.

Aidha, amesema wamebaini kuwepo kwa makundi mbalimbali yaliyoandaliwa kwa ajili ya kufanya vurugu na kuzuia watu kwenda kupiga kura, katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mtwara, na kwamba hatua zitachukuliwa dhidi yao iwapo watafanya matendo ya uvunjifu wa amani.