Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR limesema limeshtushwa na taarifa za vifo vya wakimbizi hao nchini Rwanda.
Msemaji wa UNHCR, Cecile Pouilly, amewataka wahusika nchini Rwanda kuhakikisha usalama wa wakimbizi baada ya maandamano yaliyokuwa yakiendelea tangu Febuari 20 kusababisha vifo na majeruhi
Taarifa zinasema kuwa mkasa huo ulitokea baada ya takribani wakimbizi 700 wa DRC kutoka kambi ya Kiziba kuandamana nje ya ofisi ya UNHCR sehemu za Karongi kupinga kupunguzwa kwa mgao wao wa chakula.





