Jumatatu , 4th Mei , 2015

Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Dr. Seif Rashid amesema kuwa tafiti zilizofanywa katika nchi 72 zimeonesha kwamba upatikanaji wa huduma muafaka za ukunga umewesesha kupunguza kiwango cha vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi.

Waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Dr.Seif Rashid

Jambo hilo linadhihirisha umuhimu wa wakunga katika kuhakikisha kwamba hakuna mama mjamzito anayepoteza maisha kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika.

Dr.Seif ameyasema hayo leo jijini Dar wakati akizungumzia mpango mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya mama na mtoto hapa nchini na kuongeza kuwa vifo hivyo vimepungua kwa wastani wa asilimia 3 kwa mwaka kuanzia mwaka 1990.

Aidha Dr. Seif ameongeza kuwa wizara itaweza kufikia malengo ya maendeleo ya milenia namba 4 na 5 yanayohusu kuboresha afya ya mama kwa kupunguza vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi kwa robo tatu na kuweza kufikia wakina mama 193 kwa kila vizazi hadi laki moja.