
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Chama cha Wakunga nchini Tanzania, Feddy Mwanga alipokuwa anafungua mkutano uliowakutanisha wakunga kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni kuelekea siku ya wakunga duniani hapo kesho.
Aidha kumeonekana kuwa na upungufu mkubwa wa wakunga wejnye taaluma nchini tanzania hali inayoppelekea mkunga mmoja kuhudumia wakinamama 15 kwa siku wakati ilitakiwa ahudumie wajawazito wanne kwa siku.
Aidha kuhusu suala la wakubnga kulalamikiwav kuwa na lugha chafu na kutokuwahudumia vizuri kinamama wajawazito Bi Mwanga amesema kuwa wanaendelea kupeana elimu ya jinsii ya kuwahudumia wagonjwa kwa upendo huku wakiandaa namna ya kuweza kuwajibishana kwa wale waytakaoonekana kufanya kinyume.