Jumatano , 11th Jan , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, linawashikilia watu watano wanaodaiwa kuwa ni majangili wakiwa na nyama ya nyati yenye uzito wa kilo 1,122 yenye thamani ya shilingi milioni 11.6.

Nyati

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa Shadrack Masija, amesema watuhumiwa hao hawakuwa na vibali halali vya uwindaji, pia wamekutwa na silaha tatu aina ya Riffle mbili ambazo ni mahususi kwa uwindaji zikiwa zimefungwa lensi na risasi 28.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori, Pori la akiba la Rwafi, wanasema wako macho kuzuia na kupambana na majangili hifadhini.

Hili ni tukio la kwanza kubwa kutokea katika pori la akiba la Rwafi la watuhumiwa kukutwa na kiasi kikubwa cha nyama ya mnyama nyati, nyama ya nyati ni nyara za serikali kisheria.